USIFUNGUE Official Banner
Kanlex Pictures

TELLING AFRICAN STORIES
TO THE WORLD.

Kanlex Pictures ni studio huru ya utengenezaji wa filamu yenye makao yake makuu Dar es Salaam, Tanzania. Tumejitolea kuvunja ukimya na kuondoa changamoto zote zilizokwamisha sinema za Kiafrika kwa miongo mingi, tukileta masimulizi halisi yenye viwango vya kimataifa, tukianza na filamu yetu fupi ya USIFUNGUE.

5 Misingi ya Mabadiliko
4K / HDR Viwango vya Sinema
TZS 1,000 M-Pesa / Tigo / Airtel

KWA MIAKA MINGI, TASNIA YA FILAMU NCHINI TANZANIA IMESHINDWA KUVUKA MIPAKA NA KUTEKA SOKO LA DUNIA KWA SABABU KUU 5:

Huu ni ukweli mchungu ambao watayarishaji wengi wameukwepa, lakini Kanlex Pictures tumeamua kuukabili moja kwa moja:

01

1. Uandishi Dhaifu Usiyozingatia Sayansi na Saikolojia ya Masimulizi

Uandishi unaoongozwa na 'vibe' badala ya muundo imara wa hadithi (story structure, story beat, hero's journey). Hadithi nyingi hazina msukumo wa ndani wa wahusika, migongano halisi wala mwendelezo wa kisaikolojia unaomteka mtazamaji kuanzia mwanzo hadi mwisho.

02

2. Performance Ndogo ya Waigizaji & Uteuzi usio wa Kipaji

Asilimia kubwa ya waigizaji wanashindwa kuvaa uhusika unaoshawishi kulingana na aina ya character waliyopewa kwenye hadithi. Sababu kubwa ni makosa ya director katika kuwaongoza castings, pamoja na uchaguaji wa waigizaji unaoangalia muonekano wa nje badala ya kipaji, kina cha hisia na nidhamu ya kazi.

03

3. Cinematography: Sayansi ya Kubadili Maono Kuwa Picha

Cinematography ni sayansi ya kubadili mswada na vision ya director kuwa picha zinazoibua hisia. Tamthilia iliyoongozwa na waandaji wa Hollywood kama 'Siri ya Mtungi' ilifanya kazi nzuri ya kipekee kwenye Cinematography, lakini kwa namna moja au nyingine waandaji wa filamu wa ndani walishindwa kujifunza na kuchukua maelekezo (take notes) ya kuendeleza viwango hivyo.

04

4. Sound & Music: Moyo wa Hisia na Mazingira ya Sinema

Matumizi ya sauti na muziki yana athari kubwa zaidi kwenye hisia (mood) ya scene au hadithi nzima. Sinema nyingi zimekuwa zikipuuza muundo wa sauti (sound design), kurekodi sauti safi ya mazungumzo (dialogue clarity), kelele halisi za mazingira (foley/atmosphere) na muziki maalum uliotungwa kuakisi matukio badala ya kuweka nyimbo kiholela.

05

5. Post-Production & Uhariri: Sayansi ya Rangi na Mtiririko

Filamu inazaliwa mara ya tatu chumba cha uhariri (editing room). Kutozingatia mtiririko wa ukataji picha (rhythm & pacing), sayansi ya rangi za kisasa (cinematic color grading) na viwango vya kimataifa vya master ya picha kumeziacha sinema nyingi zikionekana kama video za simu badala ya kazi ya sinema.

TAMKO LA KANLEX PICTURES

KWA KUONA HAYO, KANLEX PICTURES TUMEJIFUNZA KIPI KINAFANYA KAZI KWA KUKUMBATIA HII MISINGI YOTE:

Uandishi unaofuata Sayansi na Saikolojia ya Masimulizi Cinematography ya Viwango vya Kimataifa Uteuzi Makini na Uongozaji wa Waigizaji (Casting) Muundo Imara wa Sauti na Muziki (Sound & Music)

Tunaamini kwa kufuata hii misingi mama, tunaweza kusimulia Hadithi za Afrika kwenye global stage. Safari yetu inaanza rasmi na filamu yetu ya kipekee ya kusisimua: USIFUNGUE.

Shuhudia Kazi Yetu: USIFUNGUE ↓

USIFUNGUE — OFFICIAL TEASER

USIFUNGUE — Official Teaser Trailer Auto-Optimized

KANLEX PLAY — SINEMA MKONONI MWAKO

Tazama filamu zote za Kanlex Pictures mahali popote, wakati wowote bila kutumia bando kubwa. Mfumo wetu wa Data Saver (360p hadi 1080p FHD) unahakikisha hata kwa kifurushi cha kawaida cha simu unapata picha angavu bila kukwama.

TZS 1,000 kwa Kila Filamu
Malipo ya Haraka ya M-Pesa, Tigo, Airtel
Inalinda Bando (Data Saver Edge)

Jinsi ya Kuanza Kutazama

Hakuna usajili mgumu. Ingiza namba yako ya simu, chagua filamu ya USIFUNGUE, lipia TZS 1,000 kupitia simu yako, na anza kutazama papo hapo!

Tazama Sasa Kwenye Simu

WASILIANA NA KANLEX PICTURES

Kwa masuala ya usambazaji, maonyesho ya sinema, tamasha za filamu (festivals) au ushirikiano wa kikazi.

Ofisi na Makao Makuu

Kanlex Pictures inashirikiana na waongozaji, waandishi, waigizaji na wawekezaji wenye maono ya kubadilisha tasnia ya sinema Afrika Mashariki na kuipeleka katika majukwaa ya kimataifa.

Barua Pepe Rasmi
kanlexpictures@gmail.com
Eneo la Studio
Dar es Salaam, Tanzania
Tovuti Rasmi
kanlexpictures.com
HAKI ZA USAMBAZAJI & TAMASHA

Kwa makubaliano ya haki za maonyesho ya USIFUNGUE au miradi inayofuata, tuandikie barua pepe yenye mada '[Distribution Inquiry]'.

Tuma Ujumbe Moja kwa Moja